MAANA_YA_URASIMI.docx - MAANA YA URASIMI Kulingana na...

This preview shows page 1 - 2 out of 5 pages.

MAANA YA URASIMI Kulingana na Kezilahabi (1983), urasimi ni wakati ambapo misingi maalum ya kazi za Sanaa huwekwa na kukubalika kwa vipimo bora vya kazi nyinginezo za kisanaa. Nadharia hii ya urasimi mkongwe ina kanuni za kimsingi na za kale ambazo zilitumika kuwekea mizani tungo za awali ili kutambua ubora wa kazi hizo au udhaifu wake. USULI Nadharia hii ni miongoni mwa nadharia madhubuti kwa kuwa haina waasisi mahususi lakini mihimili yake imeweza kutokana na malighafi ya data ya kazi za kirasimi. Nadharia madhubuti ni ile inayotokana na majaribio dhabiti ambapo majaribio hayo yanaweza kufanyika katika maabara au maktaba ingawaje wanafasihi wengi huusika Zaidi na maktaba. Kulingana na R.M Wafula na Kimani Njogu katika kitabu chao ‘ Nadharia za Uhakiki wa Fasihi(2007), wanadai kwamba huenda Mwengo Bin Athumani ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika katika lugha ya Kiswahili katika utenzi wake wa Tambuko au Chuo cha Herekali (1728). Kuna utenzi wa Al-nkishafi ulioandikwa na S. Abdalla Ali bin Nasir. Huu ni utungo wa kidini ambao mwandishi anauonya moyo wake usifuate raha za kilimwengu bali aandamane na mambo yanayomhusu Mungu. Vile vile kuna ule wa Mwanakupona, utenzi ulioandikwa na mwanamke mzaliwa wa Pate na baadaye akahamia Lamu. Alikuwa mkewe Bwana Mataka ambaye alikuwa mfalme wa Siu wa wakati ule. Mwanakupona alitunga utenzi huu kumpa bintiye (Mwana Hashima) mafunzo ya namna ya kuishi na mumewe kwa kumtii na kusikiza amri yake kulingana na sharia za kiislamu na pia, jinsi ya kutangamana na marafiki, ndugu nan a watu wa aina mbalimbali. Isitoshe kuna Mashairi ya Muyaka yaliyotungwa na Muyaka wa Muhaji.

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture