PIJINI NA KIRIOLI-1.docx - Utangulizi Maana ya istilahi ya...

This preview shows page 1 - 2 out of 10 pages.

Utangulizi Maana ya istilahi ya pijini na krioli.Kwa mujibu wa mtandao [the17]Kuna mitazamo tofauti kuhusu etimolojia ya istilahi ya pijini. Hata hivyo hakuna mtazamo ambao umeweza kukubalika na wasomi katika jamii. Kwanza inaaminika kuwa dhana yapijini ni neno linalotokana na neno la kichina lenye maana ya biashara. Kwa maana kuwa istilahi hii ilitokana na sababu za kufanya biashara. Pili inaaminika pia kuwa neno hili lilitokana na neno la kireno ‘ocupao’ lenye maana ya kazi au taaluma. Wazo hili linashadidiwa na sababu kuwa wareno ndio waliokuwa wafanyibiashara wakwanza kufika kwa mataifa yanayoendelea kiuchumi na kuathiri lugha za wenyeji kwa lugha yao. Mabadiliko ya kifonetiki kutoka kwa neno asili hadi neno la sasa la pijini hayaelezeki.Istilahi ya krioli haina utata sana kama ilivyo istilahi ya pijini. Istilahi hii inatokana na neno la kifaransa ‘criollo’ ambalo linarejelea mzizi wa neno la ‘iberian’ lenye maana ya kuuguza, lea ama zalisha. Maana ya sasa ni ya wenyeji ama watu wa taifa fulani. Asilia istilahi hii ilitumika katika karne ya 17 kurejelea lugha ya mataifa ambayo yalitawaliwa na mataifa ya bara uropa. Baadaye ilipata mabadiliko ya kisemantiki na kuwa na maana ya itikadi na lugha za mataifa ya kikoloni na baadaye lugha yoyote iliyotokana na pijini zilizokuwa na msingi wake katika lugha za bara uropa. Kwa mfano kiingereza, kifaransa, kireno na kihispania.Pijini ni lugha ambayo huibuka ili kufanikisha mawasiliano kati ya jamii mbili ambapo moja ni jamii ambayo imeimarika kuliko jamii nyingine. Ile jamii ambayo haijaimarika ndiyo huibua lugha ya pijini. Kihistoria pijini ziliibuka wakati wa ukoloni ambapo wawakilishi wa wakoloni fulani, wafanyibiashara, na mabaharia walitangamana na wenyeji.Hali hii iliibua lugha ambayo ilikuwa na misingi yake kwenye lugha za wakoloni pamoja na lugha za wenyeji. Lugha hiyo ilijikita katika sababu zilizoifanya lugha hiyo kuibuka hasa mawasiliano na wakoloni. Baada ya mpwito wa wakati lugha hiyo huweza kuwa changamano hasa baada ya kuwa na wazawa wake.Lugha inapokuwa na wazawa wake huitwa krioli. Krioli ni pijini iliyokomaa. PIJINI.Kwa mujibu wa[Mat07] pijini ni lugha inayozuka panapo mtagusano au mwingiliano wa watu wanaozungumza lugha tofauti. Ni lugha iliyobuniwa na kutumiwa kwa mawasiliano baina ya watu ambaowanazungumza lugha tofauti na hawana lugha moja wanayoielewa wote.Kwa mujibu wa [Bul06]pijini ni zao la lugha mbili zilizokutana. Pijini huweza kuzuka mahali ambapo kuna makundi mawili au Zaidi na kila kundi likiwa na lugha yake. Ili kufanikisha mawasiliano, lugha hizi huchanganyika na kuingiliana kupelekea kuzuka lugha ya mchanganyiko ambayo inaeleweka na makundi yote mawili. [Msa09]nao wakiwanukuu de camp (1971) na Hall (1972) wanasema kuwa pijini ni lugha yenye mfumo uliorahisishwa sana ambao hutumiwa na wazungumzaji wenye lugha tofauti katika mazingira maalumu baina yao na kwamba pijini siyo lugha mama kwa mzungumzaji yeyote.

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture