PENDO LA KWANZA

PENDO LA KWANZA - Go rock exam yay! 1 PENDO LA KWANZA...

Info iconThis preview shows pages 1–3. Sign up to view the full content.

View Full Document Right Arrow Icon
Go rock exam yay! 1 PENDO LA KWANZA Ilikuwa jira la Kinyamajani, katikati ya Mwezi wa Kumi. Siku hii, nje kulikuwa baridi. Si baridi kali, lakini lilikuwa la kutosha la kuvaa sweta au koti jembamba. Rangi ya majani ya miti ilikuwa imeshaanza kubadilika kuwa rangi tafauti tafauti kama rangi za zambarau, kahawa, manjano, machungwa, nyekundu, hudurungi, na wardi. Ilikuwa kama saa tisa na nusu mchana na jua lilikuwa linan'gara. Mbinguni hakukuwa na mawingu. Miale ya jua ilin'garisha rangi za majani na kuzifanya na min'garo ya kuvutia na kupendeza. Upepo mwembamba ulitingisha matawi pole pole na majani kupepea. Ingawa upepo ulikuwa wa baridi, lakini haukuhisika kwa sababu ya joto la jua. Mtembezi, (ni jina la mwanamumu huyu), alikuwa anatoka kwenye jengo la Chuo cha Sheria hapa kwenye Barabara ya Amsterdam na 116. Alisimama kwenye kona akingojea taa ya barabara kubadilika kuwa rangi ya kijani. Leo alikuwa amechoka kwa sababu alikuwa ameanza kazi kutoka saa moja asubuhi alipofika affisini kwake. Aliamka mapema sana na pia alichelewa kulala kwa ajili ya matarisho ya kufundisha semina juu ya Sheri na Haki katika Nchi za Afrika Mashariki. Baada ya dakika chache, taa zilibadilika. Mtembezi akavuka barabara na kuelekea
Background image of page 1

Info iconThis preview has intentionally blurred sections. Sign up to view the full version.

View Full DocumentRight Arrow Icon
Go rock exam yay! 2 sehemu za Broadway. Alitembea pole pole. Kwenye sehemu hii ya Chuo Kikuu cha Kolumbia wakati huu kulikuwa na watu wengi wanapita. Watu wengine walikuwa wanafunzi, wengine walikuwa wafanya kazi na wengine walikuwa mamama na mababa wanaorudi majumbani kwao na watoto wao ambao walikuwa wanatoka mashuleni. Watu wengine walitembea pole pole na wengine walitembea kwa haraka wakiendea madarasani au nyumbani. Mtembezi aliendelea kutembea pole pole akilipita Jengo la Hamilton. Alipofika katikati ya sehemu ya uwanja akasikia sauti inamwita, "Mtembezi !! Mtembezi !!" Ilikuwa sauti ya mwanamke. Hakujua nani alikuwa anamwita. Akaguka sehemu ya kulia kulikokuwa Maktaba ya Maani. Akamwaona mwanamke anampungia mkono. Akasimama kumtazama yule mwanamke. Hakumtambua.
Background image of page 2
Image of page 3
This is the end of the preview. Sign up to access the rest of the document.

This essay was uploaded on 04/06/2008 for the course SWHL 2420 taught by Professor Nanji during the Spring '08 term at Columbia.

Page1 / 7

PENDO LA KWANZA - Go rock exam yay! 1 PENDO LA KWANZA...

This preview shows document pages 1 - 3. Sign up to view the full document.

View Full Document Right Arrow Icon
Ask a homework question - tutors are online