Muhimu kujadili mbinu mbalimbali ambazo hutumiwa

This preview shows page 67 - 69 out of 86 pages.

muhimu kujadili mbinu mbalimbali ambazo hutumiwa kuunda istilahi mpya za Kiswahili kwa ajili ya kutosheleza mawasiliano katika nyanja mbalimbali. Kwa ambavyo somo hili linahusu uundaji wa istilahi katika Kiswahili, ni muhimu turejelee pia visawe vya istilahi hizo katika lugha za kigeni kama vile Kiingereza. Ni muhimu kutafsiri istilahi hizo kwa sababu ‘tafsiri’ ni miongoni mwa mbinu za uundaji wa msamiati na istilahi (Tazama mbinu nambari ‘D’). Kwa ambavyo tafsiri huhusisha matumizi ya maneno ya lugha mbili tofauti, itabidi tutumie maneno mengi ya Kiingereza katika somo hili ili liweze kueleweka vilivyo (hata kama hii ni kozi ya Kiswahili). Kulingana na Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI, 1981:187), ‘msamiati’ ni jumla ya maneno yanayotumiwa na watu katika lugha. Nayo Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (TUKI, 1990:56) inaeleza kwamba, ‘istilahi’ ni mfumo wa msamiati maalum unaotumiwa katika uwanja fulani mahsusi. Katika Kiingereza, msamiati ni ‘vocabulary’ ilhali istilahi ni ‘terminology.’ Ukuzaji wa msamiati na istilahi ni jambo la kawaida katika lugha zote. Maneno mapya huundwa katika lugha ili kutosheleza mahitaji ya mawasiliano. Tatizo kubwa linalozuia matumizi ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali za maisha ni ukosefu wa istilahi za kutosha. 63
6.1 Madhumuni Baada ya kulipitia somo hili, ninatarajia kwamba utaweza: (i) Kufafanua mbinu mbalimbali zinazotumiwa kuundia msamiati na istilahi za Kiswahili. (ii) Kueleza matatizo yanayokumba uundaji wa istilahi za Kiswahili na jinsi yanavyoweza kutatuliwa. 6.2 Mbinu za Uundaji wa Msamiati na Istilahi Watafiti wengi wa Kiswahili wamezungumzia mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa kuundia msamiati na istilahi za Kiswahili. Hawa ni pamoja na Mbughuni (1989:103-109), Tumbo-Masabo na Mwansoko (1992), Kiango (1995:46-54), Chimerah (1998b) na wengineo. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu hizo: (A) URADIDI (TAKRIRI ) Ni urudiaji wa neno zima au sehemu ya neno hilo ili kupata neno jipya lenye maana tofauti. Mifano ni kama ifuatayo: Nyoko --- Nyokonyoko Tinga --- Tingatinga Bata --- Batabata Mbele --- Kimbelembele (B) UPANUZI WA MAANA Ni kulipatia neno fulani maana mpya katika matumizi. Maana mpya huwa kama kivuli cha maana asili ya neno hilo. Mifano ni kama ifuatayo: (i) Kifaru : Maana asili --- Aina ya mnyama mkubwa tena mkali afananaye na kiboko na mwenye kipusa usoni. Maana mpya --- Gari la chuma la kivita lenye mzinga. (ii) Kupe : Maana asili --- Mdudu mdogo agandaye mwilini na kufyonza damu ya wanyama. Maana mpya --- Mnyonyaji; mtu aishiye kwa jasho la wengine. (iii) Kigogo : Maana asili --- Kipande kikubwa cha mti ulioanguka au kukatwa. Maana mpya --- Mtu mwenye madaraka makubwa mahali pake pa kazi; au kiongozi wa ngazi ya juu. (iv) Mkereketwa : Maana asili --- Kukereketa ni kuasha kooni au kinywani. Mara nyingi kitu kinapomwasha mtu, huwa kinamuudhi. Maana mpya --- Mtu aliyetopea katika ushabiki wa chama, itikadi, dini, na kadhalika, ambaye anaudhiwa na changamoto kutoka kwa wapinzani wake.

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture