Maana mpya huwa kama kivuli cha maana asili ya neno

This preview shows page 68 - 71 out of 86 pages.

Ni kulipatia neno fulani maana mpya katika matumizi. Maana mpya huwa kama kivuli cha maana asili ya neno hilo. Mifano ni kama ifuatayo: (i) Kifaru : Maana asili --- Aina ya mnyama mkubwa tena mkali afananaye na kiboko na mwenye kipusa usoni. Maana mpya --- Gari la chuma la kivita lenye mzinga. (ii) Kupe : Maana asili --- Mdudu mdogo agandaye mwilini na kufyonza damu ya wanyama. Maana mpya --- Mnyonyaji; mtu aishiye kwa jasho la wengine. (iii) Kigogo : Maana asili --- Kipande kikubwa cha mti ulioanguka au kukatwa. Maana mpya --- Mtu mwenye madaraka makubwa mahali pake pa kazi; au kiongozi wa ngazi ya juu. (iv) Mkereketwa : Maana asili --- Kukereketa ni kuasha kooni au kinywani. Mara nyingi kitu kinapomwasha mtu, huwa kinamuudhi. Maana mpya --- Mtu aliyetopea katika ushabiki wa chama, itikadi, dini, na kadhalika, ambaye anaudhiwa na changamoto kutoka kwa wapinzani wake. 64
(C) UTOHOZI Ni kuyapatia maneno yaliyokopwa matamshi na maandishi ya lugha pokezi. Mifano ni kama ifuatayo: Office --- Ofisi au Afisi Bicycle --- Baiskeli Bank --- Banki au Benki Television --- Televisheni Census --- Sensa. Waqt ( Kiarabu ) --- Wakati Hakim ( Kiarabu ) --- Hakimu (D) KUTAFSIRI Katika mbinu hii, maana ya neno lililokopwa hutolewa kwa lugha nyingine, yaani lugha pokezi. Mifano ni kama ifuatayo: Right Angle --- Pembemraba Beanfly --- Nziharage Armyworm --- Viwavijeshi Bud disease --- Ugonjwa wa vichomozi Safety Period --- Kipindi Salama Secondary School --- Shule ya Upili Absurd --- Ubwege Dialogism --- Usemezo Deconstruction --- Udenguzi Leader of the Opposition --- Kiongozi wa Upinzani Scramble for the Presidency --- Kinyang’anyiro cha Urais (E) UFUPISHAJI Ufupishaji wa Akronimu ni uunganishaji wa sehemu ya kwanza ya maneno mawili au zaidi. Mifano ni kama ifuatayo: UKIMWI --- Upungufu wa Kinga Mwilini CHAKITA --- Chama cha Kiswahili cha Taifa WAKITA --- Waandishi wa Kiswahili wa Taifa TUKI --- Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili GAREX --- Garissa Express KAMATA --- Kampuni ya Mabasi Tanzania KAUDO --- Kampuni ya Usafiri Dodoma SHIHATA --- Shirika la Habari Tanzania Vifupisho vingine ni kama vile FAO, UNICEF, NATO, UNEP,na UNESCO. (F) UHULUTISHAJI Ni kuunganisha visehemu mbalimbali vya maneno mawili au zaidi ili kubuni neno moja la mchanganyiko. Kwa kawaida sehemu ya mwanzo ya neno la kwanza huunganishwa na sehemu ya mwisho ya neno la pili, kwa mfano: Runinga --- (Ru nunu + Maninga ), yaani ‘Television.’ Katika Kiswahili cha zamani, ‘Rununu’ ni sauti inayosikika kutoka mbali, na ‘Maninga’ ni macho yanayoona mbali. 65
Tarakilishi --- Mtambo au mashi ni inayopanga tara kimu kama akili , yaani ‘Computer.’ Utandaridhi --- Uta maduni unaotanda ardhi , yaani ‘Globalization.’ Msikwao --- M tu asi ye na kwao , yaani ‘Vagrant’ au ‘Vagabond.’ Chajio --- Cha kula cha jio ni, yaani ‘Supper.’ Chamcha --- Cha kula cha mcha na, yaani ‘Lunch.’ Fupaja --- Fupa la paja, yaani ‘Thigh bone.’ Kidukari --- Kidu du kikulacho sukari , yaani ‘Aphid.’ Kidungata --- Kidu du kinachokula unga na nta , yaani ‘Mealy bug.’ Kinyotomvu --- Ki dudu kinachonyo nya utomvu , yaani ‘Plant bug.’ Kiuwadudu --- Dawa au k emikali iuwa yo wadudu , yaani ‘Insecticide.’ Maneno ya Kiingereza yaliyoundwa kwa kuufuata utaratibu huo ni kama vile: Brunch --- Chakula kinachojumlisha Br eakfast + Lunch .

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture