Kazi kuu zinazohusiana sana na utafiti huu ni kama

This preview shows page 191 - 195 out of 272 pages.

Kazi kuu zinazohusiana sana na utafiti huu ni kama vile (Musa 1989), Ahmed (1996) na Pratty (1999), miongoni mwa nyingine. Katika utafiti wake Musa (1989), anadai kuwa .... , hata hivyo, utafiti huu haukubaliani nao kwa sababu..., na kwa hivyo, tofauti kuu katika ya kazi yake na hii ni... n,k. Hata hivyo, Ahmed na Pratty walitumia nadharia iliyo sawa na hii itakayotumika hapa (au iliyotumika hapa) ingawa mbinu zao za kukusanyia deta zilikuwa tofauto. Kwanza, Ahmed alikusanya deta kwa kutumia mibinu ya...ilhali Pratty alitumia .... Kwa upande mwingine, utafiti huu unatumia mbinu kama vile...ambazo ni tofauti kwa sababu .... nk Pia kunazo tafiti nyingine kadha zinazoshughlikia swala hili lakini kwa kuangalia mada tofauti na hii ya utafiti juu. Baadhi kama vile….zina mtazamo wa nadharia tofauti kama vile… na baadhi kama vile ...zinatumia deta za aina moja tu, hasa zile zilizochapishwa. Utafiti huu utatumia deta zilizochapishwa na pia zile za nyanjani na kwa hivyo, utategemea matokeo tofauti hasa katika...na ...
191 . Kwa sababu hizo utafiti wa sa ni tofauti kidogo na hizo zilizojadiliwa hapo juu. nk Kwa kumalizia, ni sharti machapisho au tafiti zinazopitiwa ziwe na sifa zifuatazo: (a) Zinahusiana kwa njia moja au nyingine na utafiti wa sasa. (b) Ni tafiti muhimu zenye kutambulikana kitaaluma wala sio makala yasiyokuwa na uzito wa kiakademia km. Makala ya magazetini au vijitabu visivyokuwa vya kiwango cha juu kitaaluma au kazi ambazo hazijasambazwa na kujadiliwa na wataalam wengine kama miswada ya makala na vitabu. (c) Ni bora zaidi kuhakikisha kuwa, kwa kiasi kikubwa, machapisho yanayohakikiwa si mengi sana ila yametanda eneo lote la mada inayotafitiwa. (d) Machapisho pia sharti yasiwe ya kizamani sana ilhali kazi nyingi za hivi karibuni zaidi zinapatikana. (e) Zimepangwa kwa muwala au utaratibu fulani kama vile: vitabu; tasnifu; makala katika majarida muhimuya kitaaluma; makala ambazo hazijachapishwa n.k.
192 8: Misingi ya Nadharia Utafiti wa kitaaluma ni utafiti wa kinadharia na sharti uongozwe na nadharia fualini moja au zaidi ya moja. Ni nini maana ya ‘nadharia’ ? Huu ni mkusanyiko wa mawazo unaotoa msimamo fulani kuhusu maisha ya mwanadamu katika ulimwengu huu. Ni mtazamo fulani kuhusu uhalisia wa maisha ya mwandadamu. Pengine nadharia pia inaweza kuelezwa kama wazo ambalo hutolewa ili kuthibitishwa kwa kufanyiwa majaribio ya utafiti. Kuna aina nyingi za nadharia kama vile nadharia kuu (k.m Umaksisti, Ubepari, Umilisi, Urasimu, Ubwege, na kadhalika). Nadharia zote hufungamana na kipindi maalum katika historia na hueleza maoni muhimu kuhusu maisha ya mwanadamu. Hii ndiyo sababu kila somo na kila taaluma ina nadharia zake muhimu ambazo hutoa mwongozo kwa watafiti. Kwa hivyo, kila mtafiti hulazimika kuteua nadharia yake atakayoitumia kutegemea mada na swala lake la utafiti. Kwa kila nadharia atakayoichagua, mtafiti anapaswa kuonyesha mambo muhimu yafuatayo: (a) Jina au majina ya nadharia (b) Mhasisi au Waasisi wa nadharia yenyewe
193 (c) wakati gani imeanza kutumika na mifano michache ya matumizi yake (nani katumia, wapi, lini na kwa njia gani).

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture

  • Left Quote Icon

    Student Picture